Karibu Songea Revival Church

Karibu  Songea Revival Church

Huduma za Songea Revival Church

Huduma za Songea Revival Church

Kanisa



          Jina la Kanisa:T.A.G - Songea Revival Church
              Kauli Mbiu: Tumeitwa Kumtumikia Mungu Kwa Viwango Vyenye Ubora Wa Hali Ya Juu
Kauli Ya Umisheni: Kumwandaa Kila Mwamini Hadi Awe Amejazwa Na Nguvu Za  Roho Mtakatifu Ili Awe Chombo Cha Kuwaleta Kwa Yesu Waliopotea Dhambini.
  Maono Ya Kanisa: Kuwajenga Waliofikiwa Ili Waweze Kuwafikia Wengine.

Historia Ya Kanisa:
Wazo la kuanzisha kanisa la TAG Songea Revival ilianza Julai 13, 2003 katika sebule ya nyumba ya kupanga aliyokuwa anaishi Mchungaji Seedfarm ‘A’ katika Manispaa ya Songea. Kwa wakati huo kanisa hili lilikuwa linaitwa TAG-Seedfarm. Mchungaji pamoja na familia kwa miezi 30 walitumia sebule yao kama sehemu ya kanisa kuabudia. Kwa muda huo wote kanisa lilikua hadi kufikia idadi ya washirika watatu pamoja na familia ya mchungaji mwenyewe, jumla ilifanya washirika saba.
Mara miundombinu ya kanisa kuhamia eneo jipya la Angoni Arms ilipokamilika mwaka 2006 Januari, tulihamia katika ukumbi huo wa kuabudia tarehe 12 Februari 2006
.
Kwa kujua kwamba eneo tulilopatia ukumbi ni eneo jingine na liko mbali na mahali kanisa lilikokuwa, uongozi wa kanisa kwa kushirikiana na washirika wa Kanisa hili ulimwomba Mungu ili kupata jina jingine tofauti na T.A.G-Seedfarm. Baada ya maombi kanisa lilipendekeza majina kadhaa na halafu kura zilipigwa. Kwa njia ya kura jina la kanisa lililopata kura nyingi ni TAG-Songea Revival, na ndivyo ilivy hata leo, kwamba kanisa hili linajulikana kama T.A.G - Songea Revival.
Kanisa la TAG Songea Revival lilifanikiwa kununua kiwanja cha kanisa mwaka 2010 mwezi Januari, na ujenzi ulianzamwezi Juni tarehe ya mosi, 2010. Mkono wa Bwana ulikuwa juu ya uongozi wa Kanisa hili kiasi kwamba hadi kufikia siku ya ibada ya kuweka Jiwe la Msingi jumla ya kiasi cha Tsh.  75,200,000/= zilipatikana na kutumika kwa ujenzi wa jengo lake la kuabudia.
Ibada ya kuweka Jiwe la Msingi ilifanywa na Askofu Mkuu wa Tanzania Assemblies of God, Rev. Dr. Barnabas Weston Mtokambali April 27, 2011, miezi kumi tangu ujenzi ulipoanza.
Hadi wakati huo wa kuweka jiwe la msingi, Songea Revival lilikuwa na jumla ya washirika mia moja na arobaini; (140), yaani watu wazima 80 na watoto 60, ambao kwa umoja wetu Bwana alitupatia neema ya kuanzisha ujenzi wa jengo la kuabudia. Kiasi hiuki cha fedha; yaani 75,200,000/= kimchanganuo, Tshs.21,000,000/= zilipatikana kama mkopo. Tshs.  9,700,000/= zilitoka katika mfuko wa sadaka na mafungu ya kumi ya wana–Songea Revival. Tshs.19,100,000/=  hizo zilikuwa changizo iliyofanywa na Wana Songea Revival.  Tshs 3,900,000/=  ilikuwa michango ya marafiki wa TAG–Songea Revival.   Na Tshs. 21,500,000/= ulikuwa mchango wa Mch. Fussi kama Injinia wa Jengo.  
WASHIRIKA
MAKUSANYO YA UJENZI WA KANISA
Wkubwa
Wtoto
Mkopo (Tzs)
Kikumi (Tzs)
Changizo (Tzs)
Misaada (Tzs)
80
60
21,000,000/=
21,500,000/=
19,100,000/= 
3,900,000/= 

Muundo Wa Jengo La TAG-Songea Revival
Jengo hili la Kanisa limejengwa katika kiwanja cha ukubwa wa mita za mraba 780 yaani mita 26 kwa mita 30. Kiwanja hiki kinatambuliwa kama Kiwanja No. 315 Kitalu B-B MAHENGE, ambacho kina jina la TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD-Songea Revival.
Kiwanja hiki kina Ukumbi wa jengo lenye ukubwa wa mita 13 x 27. Vyumba 7, yaani vi-5 ni ofisi za kanisa, kimoja Jiko, viwili stoo. Kila idara ina Ofisi yake. Chumba kimoja kilicho juu ghorofani kimebuniwa kuwa Cha Kulala Wageni; nacho ni Self-Contained.  Jengo lina chemba 6 za Vyoo vya kisasa. Chemba nne kwa matumizi ya Public na mbili kwa matumizi ya Private. Ndani ya jengo hili pia kuna sehemu maalum ya kubatizia waongofu wapya; inajulikana kama “Yordani”. Aidha juu kuna sehemu maalumu kwa ajili ya Projetor.

Ukumbi wa jengo umegawanyika katika sehemu mbili; sehemu ya chini na ya juu. Sehemu ya chini inaweza kuchukua viti 440 na sehemu ya juu inachukua viti 210, hivyo kufanya idadi ya watu 650 wanaweza kuketi na kubakiwa na mita 4 za uwazi kabla ya jukwaa la madhabahu ya kanisa. Kwa sasa jengo limeshaezekwa kwa bati na tunawekea madirisha ya Aluminium. Baadaye tunatarajia kufunga PVC-Ceillingboard na kuweka panga boi (Electrical Fanes) ili kufanya watu waabudu wakiwa katika tulivu katika majira ya joto. Nia na madhumuni ya kuwa na jengo kama hili si jingine ila Umisheni. Uelewa wetu ni huu: Ikiwa kama hatutaweza kulitumia jengo hili kama zana ya umisheni basi uwepo wake si baraka kwetu bali laana. Hivyo tunatazamia kwa kupitia jengo hili kujiongezea uwezo wa kumhubiri Kristo Yesu kwa maana hii; jengo hili linasimama kama kituo cha kukusanya rasilimali za kuhubiri Habari Njema za Yesu Kristo katika vijiji na miji iliyo ndani na nje ya mkoa wa Ruvuma.
 

No comments:

Post a Comment