HUDUMA ZINAZOTOLEWA:
Uongozi
wa Idara Kanisa la Songea Revival una wajibu wa kuwalea vijana na kuwapa fursa
ya kutumika katika ujenzi wa kazi ya Mungu.
IDARA YA CA’s
Mkurugenzi: Jeremia Kayanda |+25576464206 |
Kama maandiko matakatifu yasemavyo katika 2Korintho
5:20 “… tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba
Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe
na Mungu.”
Kanisa la TAG Songea Revival lina nafasi kwa ajili
ya vijana wakristo wanaopenda kumtumikia Mungu. Chama
cha vijana hawa wana fursa ya kukusanyika pamoja na kuwa na wakati wa
mashauriano yanayowaongoza kuainisha majukumu yao na kisha kuyafanyia uamuzi wa
nini watapenda kufanya katika kutimiza wajibu wao kwa BWANA.
Ni
jambo la fahari kwa vijana wa kanisa la Songea Revival ya kwamba yanawenda
sambamba na mwongozo wa idara ya CA’s Taifa. Wao kama vijana wa kanisa la
mahali pamoja wanatambua kwamba maisha sio suala la kula na kunywa pekee bali
furaha katika Roho Mtakatifu ambayo kwa hakika hiyo hutokana na kuifanya kazi ya Bwana Yesu. Kwa sababu hiyo
hasa idara ya CA’s katika kanisa la mahali pamoja wana program nyinginezo kama
ifuatavyo:-
1.
Kuna Programu
ya Uinjilisti; (CA’s Out Reach Movement)

Kwa
upande mwingine kanisa la SRC lina idara ya CA’s Huduma Ya Mashuleni. Idara
hiyo hushughulika zaidi na kutoa huduma ya injili mashuleni na vyuoni kwa kila
siku ya ijumaa mchana kwa mujibu wa ratiba ya vipindi vya duini mashuleni.
Kitengo
hiki cha huduma ya Injili mashuleni kinajumuisha shughuli za kuwafikia
wanafunzi wa shule za msingi, shule za sekondari, vyuo na vyuo vikuu vilivyopo
hapa Songea. Kitengo hiki chini ya mchungaji kiongozi wa SRC huandaa masomo ya
kibiblia
nay a kiumisheni na kuyafundisha katika madarasa yao au hata katika eneo la
hapa kanisani. Nia ni kuwapandia vijana uelewa sahihi wa kibiblia kuhusu imani
ya kweli na hivyo kuwa imara katika vipindi hivi vya mafundisho potofu
yaliyozagaa katika nchi yetu. Ni imani yetu kuwa masomo kama hayo ni hakika
yatawaandaa watumishi walei ndani na nje ya kanisa la T.A.G.
2.
Kuna Programu
ya “Kikombe
cha Imanueli”; (Immanuel Cup)
Kikombe
cha Imanuel au Immanuel Cup, ni daraja baina ya kanisa la Songea Revival na
vijana walioko mashuleni. Ni kitengo kinachohusika na michezo mashuleni. Kazi
yake kubwa ni kuratibu timu za shule ili:-
a. Kukuza
vipaji vya michezo miongoni mwa wanafunzi mashuleni.
b. Kuwajenga
wanafunzi katika hali ya ukakamavu na moyo wa kujituma
c. Kuwafanya
wanafunzi kuwa na wakati wa kujengwa katika maadili mema.
d. Kuwapa
fursa wanafunzi ya kusikiliza maneno ya Mungu.
e. Kuwajengea
wanafunzi maziungira ya kuwa wabunifu katika kutatua shida zao za kisaikolojia,
kijinsia na hata za kibayolojia.
3. Kuna
kuna Programu ya Usiku wa Wanafunzi (Campus Night
Moments)
Katika kitabu cha Mithali 4:13-15 Neno la Mungu
linasema (mstari wa 13) Mkamate sana
Elimu wala Usimwache aende zake, Mshike maana yeye nui uzima wako. (mstari.
14) Usiingie katika njia ya waovu, wala
usitembee katika njia ya wabaya. (mstari wa 15) Jiepushe wala usipite karibu nayo. Igeukie mbali ukaende zako.
Neno
la Mungu linawaasa vijana kupita mbali na njia za uovu. Na kwa kujua kwamba
hakuna kitu kinachoweza kumsaidia kijana kapambana na vishawishi vya ujana ila
ni ile nguvu itokanayo na neema ya Mungu ambayo kwa kupitia neno la Mungu
wanaweza kushinda nguvu za mabadiliko katika kipindi cha ujana.
Kama vijana ;
- Tunawasaidia vijana waliopo ndani ya kanisa letu lakini vile vile wale waliopo nje na kanisa letu, ili wote kama Sehemu ya vijana wa taifa letu wanapata fursa za kusaidiwa kimaadili, na kiroho.
- Kwa njia ya semina mbalimbali tunawajengea uwezo vijana ili waweze kuwa na msukumo wa kiujasiria-mali ili kujikwamua kiuchumi ili kuondokana na umasikini wa kipato.
- Kupitia mazungumzo ya kijamii katika michezo, riadha, vichekesho, maigizo, ngoma, vijana wanaweza kuwahudumia vijana wengine kwa njia iliyo nyepesi.
Idara
hii ya vijana ina ofisi iliyosheheni miudombinu ya kisasa kama vile, kompyuta
na printa zake, meza, kabati za kuhifadhia mafaili mbalimbali. Aidha idara hii
ina uongozi makini na thabiti. Kama
unataka kujifunza uongozi kwa vitendo na kwa nadharia au mambo mengine ya
maisha unakaribishwa. Rangi au dini yako
kwetu sio kikwazo.
Kitu
Ya Kufanyika Katika Programu Ya Usiku Wa Wanafunzi (Campus
Night)
Wanafunzi
hukusanyika pamoja mara moja kwa mwaka kwa ajili ya kuwa na usiku wa ushirika
wa pamoja, ili kupata burudiko, mapumziko, mazungumzo, na fursa ya
kubadilishana mawazo kuhusu changamoto za kielimu kupitia mwangaza uliopo
katika Neno la Mungu.
Campus
Night kwa kawaida hufanyika mwanzoni mwa au katikati ya mwezi Oktoba kila mwaka.
Sababu ya kuwa na Campus Night katika
majira hayo ni ili kwamba pawepo na ushiriki mkubwa wa wanafunzi kwa kuwa
katika majira hayo vyuo na shule ndio zinakuwa tu zimefunguliwa.
Walengwa
ni wanafunzi katika Chuo cha Ualimu Songea, Chuo cha SAUT, St Joseph
University, Open University-Ruvuma
Region, Chuo cha Waganga Wasaidizi- MATC, pamoja na Shule za Msingi na za
secondari zote zilizopo katika manispaa
ya Songea.
Ndani ya SRC idara hii
imegawanyika katika makundi matatu; nayo
ni:-
MUDA WA KUKUTANA:
1. CA’s Wajumbe
wa Injili wa SRC – Ahamisi Saa 10:00 – 12:00 jioni.
2. CA’s Vijana
Chipukizi wa SRC – Kila J’mosi Saa 03:00 – 05:00 Asub.
3. CA’s
Huduma Ya Mashuleni: Mashuleni & Vyuoni - KILA
IJUMAA MCHANA
Idara
Ya Wanafunzi Na Watoto
Ya Kanisa La SRC.
Watoto
ni Mbegu Njema kwa ajili ya kanisa la kesho. Idara hii ya watoto ni moyo wa
kanisa la SRC, tukiamini kwamba mtoto akilelewa katika njia impasayo kuiendea
hataiacha kamwe hata atakapokuwa mzee.
Ni
malengo na mtazamo wetu kwa watoto kwamba idara ya watoto inawagawanya watoto
katika makundi mawili. Kundi la kwanza ni la umri kati ya miaka 5-13, Kundi la
pili ni lile lenye umri kati ya miaka 13-17.
Kazi
za idara hii inajumuisha kupanga mipango ya kwenda kuhudumu mashuleni pamoja na
kutengeneza masomo ya Neno la Mungu kwa ajili ya kwenda kufundishia katika
mashuleni na vyuoni.
This comment has been removed by the author.
ReplyDelete